Wednesday, December 30, 2015

Paul Walker ameingia kwenye orodha ya matajiri

Mwigizaji nyota wa Fast & Furious Paul Walker ameingia kwenye orodha ya karibuni zaidi ya Forbes ya wasanii marehemu wanaopata pesa nyingi zaidi. Walker, aliyefariki katika ajali ya barabarani 2013, alijizolea $10.5m (£6.8m) mwaka mmoja uliopita na sasa yumo katika nambari tisa. Michael Jackson anaongoza kwa mwaka wa tatu mtawalia, akipokea $115m (£75m), ingawa ameshuka kutoka $140m alizojizolea 2014. Elvis Presley yumo nambari ya tatu $55m (£35.8m), naye aliyetunga filamu ya Peanuts creator Charles Schulz yumo nambari nne na $40m (£26m). Mzaliwa wa Uingereza aliye kwenye orodha hiyo ni Elizabeth Taylor katika nambari tano. Hawa hapa ndio wasanii 13 walio kwenye orodha hiyo ya Forbes:

 Michael Jackson: $115m (£75m)

Elvis Presley: $55m (£35.8m) Charles Schulz: $40m (£26m) Bob Marley: $21m (£13.7m) Elizabeth Taylor: $20m (£13m) Marilyn Monroe: $17m (£11m) John Lennon: $12m (£7.8m) Albert Einstein: $11m (£7.1m) Paul Walker: $10.5m (£6.8m) Bettie Page: $10m (£6.5m)

 source
 tubongetz.com

0 comments:

Post a Comment