Wednesday, July 8, 2015

Hivi ndio wanavyoshiriki pamoja kwenye Futari Waisilamu nchini China

chinese-muslim-brothers
Futari ni mlo ambao waislamu wengi hushirikiana kwa pamoja wakati wa jioni katika kipindi cha mfungo kwenye kipindi hiki cha Ramadhan… Kutokana na utaratibu ulivyo Futari huwa inaliwa wakati wa jioni.
Lakini kwa wenzetu wa China Futari huliwa muda tofauti na huku kwetu, wenzetu  waBeijing hufuturu mida ya saa moja na dakika arobaini usiku kwenye Msikiti wa Niujie. Lakini kabla ya kufuturu, watu huandaa vitafunwa vichache mbele ya mnara wa msikiti ambapo huwa wanaenda kusali.
chinese-muslim-sisters-preparing-iftar
Vitafunwa hivvyo ni biskuti, maandazi, tende, kashata, karanga, juice na matikiti maji, na baada ya hapo wanaingia msikitini kusali na baada ya sala wanajumuika pamoja na watu wengine msikitini hapo kwa ajili ya kupata Futari.
Ripoti ya Pew Foundation kutoka China inasema kwamba China ina idadi wa waislamu wasiopungua Milioni 23 na wengi wao huishi Kaskazini Magharibi mwa China.
Nimekusogezea picha kumi za waislamu hao kutoka Beijing kwa pamoja muda wa kufuturu.
iftar1
Matunda na vitafunwa vinaandaliwa mbele ya mnara wa msikiti.
iftar2
Matunda na vitafunwa vinaliwa kabla ya kuingia Msikitini kusali.
iftar3
Matunda na vitafunwa viko mezani.


iftar4
.
iftar5
Wakati wa sala kwenye Msikiti wa Niujie uliopo Beijing.
iftar6
.
iftar7
Sala inaendelea Msikitini.
iftar8
Wanawake wakiwa kwenye maandalizi ya futari.
iftar9
Zaidi ya watu 200 hukusanyika msikitini hapo kwa ajili ya Futari hiyo.
iftar10
.

0 comments:

Post a Comment