Futari ni mlo ambao waislamu wengi hushirikiana kwa pamoja wakati wa jioni katika kipindi cha mfungo kwenye kipindi hiki cha Ramadhan… Kutokana na utaratibu ulivyo Futari huwa inaliwa wakati wa jioni.
Lakini kwa wenzetu wa China Futari huliwa muda tofauti na huku kwetu, wenzetu waBeijing hufuturu mida ya saa moja na dakika arobaini usiku kwenye Msikiti wa Niujie. Lakini kabla ya kufuturu, watu huandaa vitafunwa vichache mbele ya mnara wa msikiti ambapo huwa wanaenda kusali.
Vitafunwa hivvyo ni biskuti, maandazi, tende, kashata, karanga, juice na matikiti maji, na baada ya hapo wanaingia msikitini kusali na baada ya sala wanajumuika pamoja na watu wengine msikitini hapo kwa ajili ya kupata Futari.
Ripoti ya Pew Foundation kutoka China inasema kwamba China ina idadi wa waislamu wasiopungua Milioni 23 na wengi wao huishi Kaskazini Magharibi mwa China.
Nimekusogezea picha kumi za waislamu hao kutoka Beijing kwa pamoja muda wa kufuturu.
0 comments:
Post a Comment