Dr. Slaa Dr Slaa katika hoteli ya Serena akiwa na walinzi wake 7, amefika na kuamua kuweka kila kitu wazi kuhusu ukimya wake. Soma hapo chini alichozungumza
Slaa: Kila mtu ana kiu ya kusikia Dr Slaa anasema nini, sijawahi kuona waandishi wengi hivi
Slaa: Wengi mnafahamu sina tabia ya kuyumbishwa, ninasimami a lile ninaloamini, ijulikane kama binadamu sina chuki na mtu
Slaa: Mimi sikuwa likizo kama mlivyoambiwa na wengine. Nimeamua kuachana na siasa tarehe 28 Julai 2015 saa 3 usiku.
Naomba ijulikane kuwa nilishiriki majadiliano ya awali juu ya ujio wa Lowassa ndani ya CHADEMA, ila sikuafiki ujio wake.
Slaa: Mchakato ndani ya CHADEMA ulianza mapema na jina langu lilipitishwa lakini bado sikuitangaza popote.
Slaa: Suala la Msingi ni kuangalia kama ni ASSET au LIABILITY, ASSET kwa maana kwamba anakuja na watu wangapi kwenye chama
Slaa: Tuliambia anakuja na wabunge wanaomaliza muda wao zaidi ya 50 na viongozi wengine toka CCM.
Slaa: Siku zikapita sikupewa majina ya wabunge hao, wenyeviti wa CCM mikoa wala makatibu wakuu.
Slaa: Upotoshwaji kwamba Dr Slaa alikubali toka mwanzo si kweli naomba viongozi wangu waseme kweli.
Slaa: Kamati kuu tumekaa toka saa 9 hadi 12:30 kikao kikavunjika, ikasemwa iundwe kamati ndogo kunishawishi, nikakataa.
Slaa: Niliandika barua ya kujizuru ndani ya kamati kuu kwa mwenyekiti wakati huo akiwa Profesa Safari, ambaye aliichana.
Slaa: Mimi mwanasiasa niliyozoea naamini siasa ni sayansi haitaki uongo, haitaki udanganyifu.
Slaa: Maamuzi yaliyofanywa, yalifanywa na mimi kwa ridhaa yangu mwenyewe.
Slaa: Sisi katika familia yetu tumezoea propaganda hizo, nishasema kama mna ushahidi muulete
Slaa: Nataka niwahakikishie D. Slaa na watoto wake wameendelea kula mihogo kama tulivyoahidi maana pesa imesaidia watanzania
Slaa:Ni lazima mwanasiasa yoyote duniani hataji jina linachafuliwe, hata Dr Slaa hataki jina lake lichafuliwe ni haki yangu.
Slaa: Jambo ambalo nataka nifafanue ni suala zima la LIABILITY au ASSET, ASSET nimelieleza, wamekuwa waongo hawakutekeleza
Slaa: Mtu ambaye hata mwezi mmoja haujapita tangu useme CCM ikimteua Lowassa atajitoa, leo anasema ni msafi.
Slaa: Wenyeviti waliokuja CHADEMA wote toka CCM ni mzigo, makapi.
Slaa: CHADEMA inachukua mtu kwa sifa ya wizi wa kura, kama hatutaki kuiba kura sisi tunaenda kufanya
Slaa: Suala la ASSET sikupata majibu, ndio maana hadi leo viongozi wangu wamepata kigugumizi, naongelea kwanini nimeondoka.
Slaa: Mimi padri , yaani nikubali kuweka mkataba na shetani kwaajili ya kuiondoa CCM? unaondoa CCM kwa ‘progamu series
Slaa: Watu waliikubali CHADEMA kwaajili ya misingi ya uadilifu, leo tuna unadilifu?
Slaa: Duniani kote tuhuma zinatolewa na ni jukumu la serikali kutoa majibu. Kama watu hawajui siasa bora wakae kimya.
Slaa: CCM siwezi kuwahurumia, hata Lowassa hapa alipofika ni kwakuwa CCM ilimlea.
Slaa: Kama ukikuta choo cha kitanzania, ukapakua kilichoko ndani ya choo na kuweka chumbani kwako, ipi ni choo?
Slaa: Mimi nilikuwepo 2008 wakati tunajadili RICHMOND tunapozungumza masuala hayo ni kwakuwa tunayajua na tuliyaishi Bungeni
Slaa: Lowassa tunamtuhumu mengi , mimi simtuhumu kwa RICHMOND tu, 2010 mimi nilimwambia atumbie hadharani RICHMOND ya nani
Slaa: Ni afadhali nipotee kwenye siasa Tanzania na duniani kote kuliko kuyumbishwa na misimamo yangu.
Slaa: Mimi nimeletewa rushwa asubuhi, nikamuuliza aliyeleta kama mimi unanipa milioni 500 unazo ngapi?
Slaa: Mwanzo wa RICHMOND lazima urudi kwanza kwenye taarifa ya baraza la mawaziri februari, 2006.
Slaa: Naomba mtambue kwamba suala hili la RICHMOND halikuanzia kwa Kikwete bali lilianzia kwa Mkapa.
Slaa: 2006 feb 10, Waziri mkuu alikuwa Lowassa, sasa leo unapokuja kunambia hakuhusika maanake nini?
Slaa: Ripoti ya Mwakyembe alitoa option mbili, Waziri Mkuu ajipime au Bunge lijadili na kutoa uamuzi, akakimbilia kujiuzulu.
Slaa: Lowassa dakika ya mwisho aliingilia, hakusaini yeye ila aliagiza personal assistance wake akasaini.
Slaa: Watu wanauliza kwanini namsema Lowassa mwenyewe ni kwakuwa anagombea urais wa nchi.
Slaa: Nendeni basi Monduli kwa Lowassa na Karatu mlinganishe wakati nikiwa mbunge, halafu tuone huyu mnayemuita mtendaji.
Slaa: Mnasema habari za shule ya kata, hizi sio zao lake ni upotoshwaji, aseme alibuni wapi wazo hili.
Slaa: Ugomvi wangu na Masha ni kwasababu nilitoka hadharani na kusema Masha umeingilia mchakato wa serikali, nikawa adui.
Slaa: Wakaandika uongo kuwa RICHMOND ni kampuni ya stationary wala sio umeme
Slaa: Waziri Mkuu anajua yote halafu ananyamaza, kama alikuwa hajui ni mzembe, kama ni mzembe hafai tena kuwa Rais wa nchi.
Slaa: Kumbuka Tanesco ni chombo kinachojitegemea, ikaagizwa kusaini mkataba ambao haikujadili, maanake ni nini?
Slaa: CHADEMA tumaini jipya lilijengekea, vijana wanaliamini ninaogopa, kwa masikitiko ninasema sitaki baadaye tufike pabaya
Slaa: Kama CHADEMA leo inafika hatua ya kujaza uwanjani watu kwa mabasi halafu mnasema kuna mafuriko,siko tayari kuwa zezeta
Slaa: Udanganyifu huu wa kujaza watu kwa kubebwa na magari kuja uwanjani wakajaza uwanja walikuwa nao CCM
Slaa: Nimewasikia CHADEMA jangwani, waliyoongea ni sehemu kubwa ya ilani ambayo ilishaandaliwa zamani, hakuna kipya.
Slaa: Kinachoniumiza ni sisi kuwa wabovu zaidi ya CCM.
Slaa: Nataka Lowassa ajue kuwa tunajua, Scotland inatuandikia kuwa achunguzwe kwa paundi milioni 400 alizopeleka marekani.
Slaa: Halafu wanasema nikizungumza eti nitaharibu sifa yangu, wacha iharibike.
Slaa: Mimi nimefundishwa kukemea maovu.
Slaa: Leo anakuja mtu hapa anatuambia nyamazeni? Mimi sitaki kuingia kwenye mambo ya akina babu seya.
Slaa: Leo baadhi ya vyuo vinatumia kesi ya babu seya kufundishia kama kesi ya ulawiti halafu lowaasa anasema ataifuta
Slaa: Nani aliyeagiza maaskari waingie na mbwa pale mwembe chai msikitini? Sumaye huyu huyu aliagiza.
Slaa: Lowassa akili yake ipimwe, kesi ya ulawiti Rais hapaswi kuingilia, anaingilia uhuru wa mahakama
Slaa: Ni afadhali kutokuwa na Rais wa aina hii, Rais ambaye anatumia udanganyifu kwakuwa watu hawajasoma hafai.
Slaa: Waswahili wanasema ukiumwa na nyoka basi hata jani ulikimbie, inabidi tuhakikishe kwamba tunakuwa makini
Slaa: Alipokuwa Waziri Mkuu haya matatizo yanayotokea leo hayakutokea?
laa: Mtu aliyesababisha migogoro ya mipaka halafu leo anataka kuwa Rais?
Slaa: Wapo watakaosema ameichana CHADEMA, ameijenga CCM. Ukweli haugawanyiki, kama yameitandika CHADEMA ndio ukweli ulivyo
Slaa: Nimesema sina chama ila mimi ni mtanzania, nitawatumikia watanzania kwa vipawa alivyonipa Mwenyezi Mungu.
Slaa: Nimeombwa kugombea urais kwenye vyama vitano ila nimekataa kwakuwa mimi siamini katika kuhama hama vyama.
Slaa: Mshenga niliyemtaja, alisema kanisa la kilutheri lote linamuunga mkono Lowassa, na maaskofu wa katoliki 30 wamehongwa
Slaa: Sitaenda chama chochote, nimesema sina chama, siasa kwa maana ya chama sina, ila siasa kwa ninayoamini.
Slaa: Sijaja kufanya kampeni leo, nimekuja kuwakumbusha Watanzania wasije wakajuta kama ambavyo tunajuta kwa kosa tulilofanya 2005 na 2010.
0 comments:
Post a Comment